UKIKUTA MKUKI NJE KWA WAMASAI KUNA MAANA GANI??
LEO NAFAFANUA.
Kwa muda mrefu Sana nimesikia dhana potofu ikisemwa na watu wasio na uelewa hata kidogo juu ya dhana ya WAMASAI Kuweka mkuki nje.
Hivi karibuni nilikuwa nasikiliza radio moja na mhubiri alikuwa anafundisha kuhusu Ndoa ghafla akalisemea hili kwa uelewa wake mdogo na kuwadanganya wasikilizaji,acha nikuambie sio tu nilichukia lakini niliona hata yote aliyotangulia kuyasema kuwa yalikuwa uongo.
Kwa kweli sipo tayari hata kumsikiliza tena siku nyingine huyo mhubiri kwani nimemhesabu kama mwongo kwa kuzungumza kitu asichokijua.
IKO HIVI;-Wamasai Ni jamii ya tofauti(sio wabantu).historia yao Ni ndefu Sana na nikipata muda nitakujuza siku nyingine.
Tabia yao ni kuishi maeneo yaliyorafiki zaidi kwa ufugaji wao huku wakihama hama kutoka eneo moja kwenda lingine kufuatana na malisho yanavyopatikana.
Kwasababu hiyo wanajikuta wakifika kwenye mazingira hatari kwao na mifugo yao kwa mfano ktk maeneo yenye wanyama wakali na wasiofugwa.
Hiyo ndiyo inayowasababisha WAMASAI kuwa na tabia ya kutenbea huku Wakiwa nanajilinda yaani Wakiwa na sime,fimbo,rungu na mkuki.
Hata hivyo wamasai Wana Mipaka ktk matumizi ya silaha hizo ikizingatia umri au rika husika.kwa mfano vijana wanapowekwa wakfu kuwa madarakani Kama rika hukabidhiwa dhamana yote ya kulinda Mali na jamii kwa ujumla hivyo wao huwa na uhalali wa kumiliki na kutembea na silaha hizo wakati wowote na mahali popote.
Uhusiano wa Mkuki na Wamasai:-Kwa Wamasai Wana masharti makubwa na magumu kwa kila rika linaloingizwa madarakani kama vile;-
1.Kila Kijana aliyepo kwenye Rika lililopo madarakani haruhusiwi kula chakula mwenyewe bila mwenzake kuwepo.hii huwasaidia hata wasio nacho kutunzika kwa walio nacho.hivyo Ni vigumu kumkuta Kijana wa kimasai akitembea peke yake hasa wawapo nyumbani.
2.Ili kutunza utaratibu na nidhamu kwa wote, kila mmoja ktk rika lake hupaswa kuwa tayari kumpokea na kumtunza mwenzake wa Rika lake Kama ni mgeni au nwenyeji ktk eneo lile.hii Ni kwa wanaume tu.hivyo Kama unesafiri na kufika eneo uendapo utatakiwa uelekezwe kwa mtu wa Rika lako ili akutunze kwa chakula na malazi.
*Hata Kama mwenyeji wako sio wa rika lako atakuelekeza mahali wale wa rika lako walipo ili utunzike kwa malazi kwani dharura inapojitokeza Kama Vita au wanyama mtapaswa kujumuika pamoja Kama jeshi lililopo madarakani.
3.Ingawa kutembea na mkuki Ni sawa,hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuingia ndani na mkuki wake.sharti ufikapo kwa mwenyeji wako hata Kama hayupo ukisha pokelewa Basi utakaribishwa ndani na Kisha wewe utaukita mkuki wako nje ya nyumba yake.hii haina Uhusiano wowote na dhana ya kipumbavu inayosemwa na wengi wasiojua desturi za Wamasai.
Baada ya kuuweka mkuki huo nje,Giza linapoingia utapaswa kuuondoa na kuupeleka pembeni ya boma na ikiwa wapo wasichana ndio watakaopaswa kuuchukua na kuupeleka mahali husika.
Pia ifahamike kuwa Wamasai ndio jamii yenye faini kubwa kwa kila anayevunja maadili kwa mwenzake au kwa mtu yeyote wa Rika lake au lililomzidi yaani mzee.hii huwafanya wasivunjiane heshima au kuibiana wao kwa wao.
Kwa leo naomba niishie hapo Ila wazungu Wana msemo usemao kwamba "ikiwa hujafanya utafiti,huna ruhusa ya kuzungumza".
Niwasihi wale wenzangu na Mimi mnisadie ku share Elimu hii isikike maana naona Uongo umechukua nafasi kubwa ktk hili.
Kumbukumbu la Blogu
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
TATIZO SIO MTAJI NI WEWE TU
Hawa ni wale wenye shauku kubwa moyoni mwao kufanya jambo la pekee na hawafanyi lakini ukiwauliza watakupangia sababu nyingi za kuhalalisha ...
-
KIMAASAI to ENGLISH pronounced hello= supai hello all = enda supai pooki thank you very much=ashe oleng' ve...
-
UKIKUTA MKUKI NJE KWA WAMASAI KUNA MAANA GANI?? LEO NAFAFANUA. Kwa muda mrefu Sana nimesikia dhana potofu ikisemwa na watu wasio na uel...
-
Jinsi ya Kuishi Maisha Yenye Furaha “Nitakuwa na furaha nikifunga ndoa na kupata watoto.” “Nitakuwa na furaha nikimiliki nyumba yangu mw...
