Hapo zamani za kale kulikuwa na boma fulani hivi la kimaasai ambae ndani mwake kumejaa watu ng'mbe mbuzi kondoo.n.k hawa ng'ombe walikuwa na ndama wadogo kuna mama moja kwenye hiyo boma alifanikiwa kupata dama mzuuri sana tena ndama dume, pia huyo mama alikuwa na msichana mwenye umri wa miaka 12 hivyo huyo msichana aliambiwa na mama kuwa yeye ndio atakuwa anakamua hiyo NG'OMBE msichana akakubali bila shida akaanza kuendelea na kazi yake ya kukamua NG'OMBE mpaka ndama alivyokua na uwezo wa kula majani, kutokana na uzuri wa huyo ndama msichana akampa jina hili LOOLTIPOT siku moja jioni msichana alipo kwenda kukamua ng'ombe akang'atwa mikono na looltipot lakini kwa bahati nzuuri hakunga'ata saana msichana Akapotesea akaenda, pi looltipot alikuwa ni ndama mpole kuliko wote kwahiyo kila ijioni watoto wote wanakuja kumchezea sana mpaka wanampanda mgongo shingo wengine wanamshika mkia wengine mdomo basi ndama alivyokjwa mpole hakimbii wala haruki yaani anatulia tu,
Siku ya pili ilipofika jioni msichana akachukuwa kibuyu kwenda kukamua akakamuaaaaa alipokaribia kumaliza looltipot akamg'ata vidole kiasi kwamba damu imemtoka kidogo yule msichana akamkimbilia na kumpiga kwa nguvu lakini looltipot alikimbia na kumuacha msichana hoi akiwa anataka kuli kwa maumivu aliopata, jioni hiyohiyo kama kawaida watoto wakaanza mchezo yao na ndama looltipot,
Siku ya tatu kama kawaida ilipofika jioni msichana akaandaa kibuyu kwenda kukamua akakamu ndama akamg'ata kidogo MSICHANA akamwaambia looltipot acha kuning'ata,nitaenda kumwaambia mama kuwa unaning'ata LOOLTIPOT akamjibu na mm nitakusema kwa baba yako kuwa una mimba
KUMBE YULE MSICHANA ALIKUWA NA MIMBA YA MIEZI 4 NA WAZAZI WAKE HAWAKUJUA KWAMBA MWANAO ANA MIMBA, NA WASICHANA WA KIMASAI WAKIBEBESHAA MIMBA KABLA HAJATAIRIWA KUNA JINA WATAKUWA WANAITA YULE MSICHANA KWASABABU AMEBEBA MIMBA YA KISICHANA JINA LENYEWE NI HILI (ENDAAPAI)
yule msichana alipoambiwa hivyo na looltipot akashtuka na kujiuliza kimya kimya huyu ndama anajua kuongea? Amejuaje nina mimba? Msichana akaacha kukamua kwa mshutuko mkubwa sana, basi yeye alivyoondoka tu watoto wakajaa pale kama kawaida na kuanza mchezo yao basi looltipot nae aliwazoea watoto kwahiyo nae anawachezea yaani watoto wakipanda kila sehemu ya mwili wake na hukimbia ili kuwaangusha wale watoto na watoto hukimbia na kusema anatupiga basi watoto wakikimbia mtoto atakao kuwa wa mwisho looltipot anammeza bila ata kutafuna basi watoto walipo rudia kumchezea looltipot hakumeza wa pili aliwachezea tu mpaka watoto walichoka wakaenda kulala basi wazazi wa yule mtoto aliomezwa waliendelea kumsubiri mtoto yao mpaka usiku kabisa walienda nyumba kwa nyumba na kuwauliza wale watoto waliokuwa wakicheza wote lakini wapi na wapi hawakupata mpaka wamelia wamefarijiwa wakatulia,
Siku ya nne kama kawaida jioni msichana akatayarisha kibuyu ng'ombe walipo fika nyumbani msichana akaanza kukamua siku hiyo alifanikiwa kumaliza bila kung'atwa akafurahi sana, kama kawaida watoto wakaanza mchezo na looltipot akafanya kama alivyofanya jana na wazazi nao hivyo hivyo tu, kwa kweli watu walishangaa sana watoto wao wanaenda wapi tena mda huu fupi tu haipo,
KUMBE YULE MSICHANA SIKU ZILE ALIPOONGELESHWA LOOLTIPOT AKAFIKIRI SANA ATAFANYAJE JUU YA HUU MIMBA? SASA MAMA YAKE HUWA KILA SIKU ANAENDA KWA MARAFIKI WAKE WA JIRANI SASA YULE MSICHANA ACHACHIMBA UVUNGUNI KWA KITANDA AKACHIMBA LISHIMO KAMA CHOO LIREFU SANA KWA KWENDA CHINI NA NI PANA KIASI, AKATAFUTA JIWE PANA KAMA MEZA AKAENDA KUWEKA KUIFUNIKIA LILE SHIMO, MAMA YAKE ALIPO RUDI HAKUONA CHOCHOTE NYUMBA YAKE NI KAMA KAWAIDA, SASA KAZI YA KUKAMUA INAENDELEA TU NA UMEZAJI WATOTO INAENDELEA TU,
LOOLTIPOT ALIKUWA MKUBWA SANA KUPITILIZA KIASI, HAKUNA ATA NG'OMBE WA KUFANANISHA KWA UNENE NA ATA KWA UKUBWA, LOOLTIPOT IKAFIKA KIWANGO AMBAE KILA MTU ANAMTAMANI KWENDA KUMCHINJA KWENYE MASHEREHE, MPAKA MAMORANI WALITAKA WABADILISHIWE KWA NG'OMBE KADHAA ILI WAPELEKE PORINI KWENDA KUMCHINJA LOOLTIPOT,
Kumbe msichana alikuwa alifanya mambo fulani ya wizi yaani kila wamorani wakija pale kwao kwa mama yake kunywa maziwa anawaibia mikuki,sime,mishale na upinde viatu vikubwa na vidogo,nguo, pia alikuwa anamwibia mama yake baadhi ya vitu kama vile ngozi ya kulalia,kuni,vibuyu,nguo,mafuta,maziwa,.n.k huyo msichana kila kitu anachoiba anatumbukiza katika lile shimo alilochimba uvunguni,
Siku moja wamorani mwa kimaasai walimjia Huyo mzee mwenye dume mkubwa mzuuri ambae kwa majina aliitwa looltipot wakamwaambia mzee tunaomba huyo dume wako kwa ng'ome 7 kubwakubwa mzee akawaambia hapana sipeani ata kwa ng'ombe kumi, wamorani wakarudi manyumbani kwao wakaaenda kufikiriaaaaa, wakarudi tena mzee tumepata hizo ng'ombe 10 mzeee akawaambia sawa pelekeni, vijana wakachukua dume asbuhiiiii kwenye saa kumi ya usiku hawa vijana walikuwa 8 wadogo watatu na wakubwa watano, wakaendelea na safari yao ya kwenda porini kula nyama kumbe sehemu wanaoenda ilikuwa mbali kidogo kwahiyo hawakuweza kufika siku hiyo, katikati ya safari wakakuta kiboma fulani cha kizamani wenyewe walihamaga vijana wakasema tulale hapa ili kesho asbuhi na mapema tunaondoka, wakakubaliana kwenye ile kiboma kuna vijinyumba viwili vya majani sawa wale vijana wakagawanyika wadogo wakalale sehemu yao na wakubwa kwa sehumu yao, ilipofika kwenye saa sita usiku looltipot akawa anajikuna na kile kijinyumba waliolala vijana wadogo looltipot alijikuna mpaka anataka kuangusha kile kijinyumba
Dogo moja amamwaambia mwenzake aende kumpiga ndume anaetaka kuangusha nyumba mwenzake akaenda kupiga looltipot aache kujikunia nyumba ile alipotaka kumpiga tu looltipot akameza, na akaendelea kujikuna na nyumba, wenzake waliopo ndani wakazani alikuwenda kwa wakubwa mingine kwenda kumpiga akamezwa yule moja aliobaki akasema hawa vipi wananiacha mimi peke yangu, na huyu looltipot na anatuletea shida ya kujikunia na nyumba c atatuangushia dogo kwa hasira skachukua fimbo kwenda kumpiga looltipot akameza ata kabla ya kuachia fimbo,
KUMBE LOOLTIPOT ALIKUWA AMEWAHISABU HAWA VIJANA
basi akajikuna na ile kibanda mpaka amezambaratisha kuhakikisha kwamba hajabakiza chochote alipomaliza akahamia kwa wakubwa akaanza kujikuna na kibanda wale vijana wakubwa wakafanya kama wadogo yaani moja baada ya mwenzake na wao pia hudhani kwamba wengine wanaenda kule kwa wadogo looltipot akawala wale watu nane kisha akazambaratisha boma yoote, alipo akikisha kwamba hamna watu akapunzika ilipofika saa kumi usiku akaanza safari ya kurudi nyumbani amekuwa mbabe balaa yaani ananguruma tu kila saa,
Kumbe kule nyumbani yule msichana mwenye mimba aliingia kalika lile shimo lake alilochimba uvunguni na kwenda kujifungulia mule ndani bahati nzuri amejifungua mapacha wawili tena wote ni wa kiume,
Looltipot akafika nyumbani asbuhi na mapemaaa ananguruma tu, akaja mpaka kwao watu walishangaa huyu dume alipenyaje watoto wetu wakwaapi wakati huo hakuna cha simu wala nini, wazazi wa wale vijana wakasubiri vijana wao kama watarudi lakini hawakurudi walienda kufuatilia kutafuta lakini wapi na wapi hawakupata,
Kumbe yule msichana aligundua tu yule ndama ni mnyama hatari sana ndo maana anaandaa mapema kujificha, siku hiyo usiku kwenye mida ya saa tano usiku akaanza kuwala watu wa Boma lake anafamia nyumba baada ya nyumba ilipofika ile nyumba yao akala mama baba watoto lakini hakufankkiwa kumpata yule msichana aliemlea akasambaratisha nyumba lakini wapi na wapi hakumpata, akala majirani woote yaani kwenye kijiji hicho hajabakiza ata MTU moja wala mtoto, .
Alipomaliza zoezi yake ya siku moja akaja kupunzika chini ya mti bonge la dume, kwenye zile maboma kitu kilichobaki ni ng'ombe na mbuzi na kondoo,
Basi yule msichana aliekwenda kuishi kwenye shimo akiwalea wale mapacha yake mpaka wamekuwa wakubwa mama yao akawafundisha namna ya kutumia zile zilaha zoote mpaka wale mapacha hawataki kuishi tena ndani ya shimo, mama yao aliwaelezea mambo yoote yaliyofanyika mule, wale mapacha wakawana hasira sana na huyo mnyama loolripot, kila siku kukikucha ng'omevwanaenda wenye porini kula majana pamoja na kiongozi yao looltipot, na baadae kurudi tu wenyewe, kila siku tu kukikucha yule mwanamke wanatoka ndani ya shimo kutembea tembea na kufana mazoezi ikifika mda wa saa kumi jioni ambapo ng'ombe na mfalme wanarudi home, na wao wanarudi ndani ya shimo, basi wale mapacha wakawa wakubwa sana kiasi kwamba wana uwezo wa kumuuwa looltipot.
Siku moja mama yao akawaruhusu kumuua akawaelekeza namna na ujanja akawapa kila aina ya silaha mishale mkuki sime n.k kumbe alikuwa aliwatengenezea mapacha wake kinyumba juu wa ule mti ambae looltipot anakuja kujipunzisha, mama akawaambia wanao pandeni juu wa mti mkakae kule kwenye nyumba niliowaandalia akawafundisha kabisa namna ya kumuua ilipofika saa nane mwanamke yeye akarudi ndani ya shimo na kujifungia, basi kama kawaida ilipofika mda wa saa kumi jioni LOOLTIPOT akaja kupunzika chini wa ule mti basi wale mapacha wakaachi mishale mikuki mapanga mashoka mavisu kusema ukweli looltipot akauwawa palepale chini wa mti na mapacha wakashuka na kumuita mama yao kuwa wamemaliza kazi mama kwa furaha na machozi yakidondoka akapanda juu kisha akwakumbatia na kuwalilia sana na kusema hivii ASANTENI SANA WANANGU KWA KUOKOA MAISHA YANGU SIKUWA NA UHAKIKA KAMA MTAIWEZA HII KAZI ASANTENI SANAAAAAA.
ninaishia hapa kwa siku ya leo asanteni ila msisahau kushare kwa wenzenu