Hawa ni wale wenye shauku kubwa moyoni mwao kufanya jambo la pekee na hawafanyi lakini ukiwauliza watakupangia sababu nyingi za kuhalalisha kwa nini hawawezi kuanza na wala hawafanyi jitihada yoyote kuanza kuishi kile wanachosikia moyoni.
nepasnay
Kumbukumbu la Blogu
Alhamisi, 18 Agosti 2022
TATIZO SIO MTAJI NI WEWE TU
Hawa ni wale wenye shauku kubwa moyoni mwao kufanya jambo la pekee na hawafanyi lakini ukiwauliza watakupangia sababu nyingi za kuhalalisha kwa nini hawawezi kuanza na wala hawafanyi jitihada yoyote kuanza kuishi kile wanachosikia moyoni.
Jumamosi, 21 Machi 2020
UKIKUTA MKUKI NJE KWA WAMASAI KUNA MAANA GANI??
LEO NAFAFANUA.
Kwa muda mrefu Sana nimesikia dhana potofu ikisemwa na watu wasio na uelewa hata kidogo juu ya dhana ya WAMASAI Kuweka mkuki nje.
Hivi karibuni nilikuwa nasikiliza radio moja na mhubiri alikuwa anafundisha kuhusu Ndoa ghafla akalisemea hili kwa uelewa wake mdogo na kuwadanganya wasikilizaji,acha nikuambie sio tu nilichukia lakini niliona hata yote aliyotangulia kuyasema kuwa yalikuwa uongo.
Kwa kweli sipo tayari hata kumsikiliza tena siku nyingine huyo mhubiri kwani nimemhesabu kama mwongo kwa kuzungumza kitu asichokijua.
IKO HIVI;-Wamasai Ni jamii ya tofauti(sio wabantu).historia yao Ni ndefu Sana na nikipata muda nitakujuza siku nyingine.
Tabia yao ni kuishi maeneo yaliyorafiki zaidi kwa ufugaji wao huku wakihama hama kutoka eneo moja kwenda lingine kufuatana na malisho yanavyopatikana.
Kwasababu hiyo wanajikuta wakifika kwenye mazingira hatari kwao na mifugo yao kwa mfano ktk maeneo yenye wanyama wakali na wasiofugwa.
Hiyo ndiyo inayowasababisha WAMASAI kuwa na tabia ya kutenbea huku Wakiwa nanajilinda yaani Wakiwa na sime,fimbo,rungu na mkuki.
Hata hivyo wamasai Wana Mipaka ktk matumizi ya silaha hizo ikizingatia umri au rika husika.kwa mfano vijana wanapowekwa wakfu kuwa madarakani Kama rika hukabidhiwa dhamana yote ya kulinda Mali na jamii kwa ujumla hivyo wao huwa na uhalali wa kumiliki na kutembea na silaha hizo wakati wowote na mahali popote.
Uhusiano wa Mkuki na Wamasai:-Kwa Wamasai Wana masharti makubwa na magumu kwa kila rika linaloingizwa madarakani kama vile;-
1.Kila Kijana aliyepo kwenye Rika lililopo madarakani haruhusiwi kula chakula mwenyewe bila mwenzake kuwepo.hii huwasaidia hata wasio nacho kutunzika kwa walio nacho.hivyo Ni vigumu kumkuta Kijana wa kimasai akitembea peke yake hasa wawapo nyumbani.
2.Ili kutunza utaratibu na nidhamu kwa wote, kila mmoja ktk rika lake hupaswa kuwa tayari kumpokea na kumtunza mwenzake wa Rika lake Kama ni mgeni au nwenyeji ktk eneo lile.hii Ni kwa wanaume tu.hivyo Kama unesafiri na kufika eneo uendapo utatakiwa uelekezwe kwa mtu wa Rika lako ili akutunze kwa chakula na malazi.
*Hata Kama mwenyeji wako sio wa rika lako atakuelekeza mahali wale wa rika lako walipo ili utunzike kwa malazi kwani dharura inapojitokeza Kama Vita au wanyama mtapaswa kujumuika pamoja Kama jeshi lililopo madarakani.
3.Ingawa kutembea na mkuki Ni sawa,hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuingia ndani na mkuki wake.sharti ufikapo kwa mwenyeji wako hata Kama hayupo ukisha pokelewa Basi utakaribishwa ndani na Kisha wewe utaukita mkuki wako nje ya nyumba yake.hii haina Uhusiano wowote na dhana ya kipumbavu inayosemwa na wengi wasiojua desturi za Wamasai.
Baada ya kuuweka mkuki huo nje,Giza linapoingia utapaswa kuuondoa na kuupeleka pembeni ya boma na ikiwa wapo wasichana ndio watakaopaswa kuuchukua na kuupeleka mahali husika.
Pia ifahamike kuwa Wamasai ndio jamii yenye faini kubwa kwa kila anayevunja maadili kwa mwenzake au kwa mtu yeyote wa Rika lake au lililomzidi yaani mzee.hii huwafanya wasivunjiane heshima au kuibiana wao kwa wao.
Kwa leo naomba niishie hapo Ila wazungu Wana msemo usemao kwamba "ikiwa hujafanya utafiti,huna ruhusa ya kuzungumza".
Niwasihi wale wenzangu na Mimi mnisadie ku share Elimu hii isikike maana naona Uongo umechukua nafasi kubwa ktk hili.
Ijumaa, 8 Novemba 2019
JIFUNZE BAADHI MAJINA YA VITU MBALIMBALI KWA LUGA YA KIMAASAI
KISWAHILI. KIMAASAI
Ng'ombe. Enkiteng'
Mbuzi. Enkine
Kondoo. Enkerr
Punda. Osikirria
Paka. Embuus
Pundamulia. Oloitiko
Mbogo. Olorro
Tembo. Arkanjawoi
Swala. Enkoilii
Fisi. Orng'ojine
Chui. Orkedi
Twiga. Ormeut
Sungura. Enkitejo
Konokono. Olosiki
Chura. Entwaa engare
Kuku. Enkuku
Panya. Enderoni
Nyoka. Alasurai
Kobra. Entara
Nyumbu. Oingat
Mbuni. Esidai
Sokwe mtu. Kukuu tung'ani
Ngiri. Orbitirr
Nguruwe. Enkurupe/orkupe
Nyani. Oltulal
Mangei. Endere
MAJINA YA VYAKULA
Mahindi. Irpaek
Maharage. Irmaragi
Mchele. Ormushele
Maji. Enkare
Uji. Euji
Ugali. Argali
Viazi. Irmurungu
Nyama. Inkiri
Maziwa. Kule
Kirunguu. Enkitunkuu
Nyanya. Inyanya
Maembe. Irmaembe
Mayai. Irmosoor
Matunda. Irng'anayok
Mafuta. Eilata
Mwiko. Ormertie
Kijiko. Enkijiko
Ukoko. Enkaoji
Boga. Olokunku
Mnafu. Imbenek oormomo
Makande. Irpaek oidong'o
Ndizi. Indisi
Karot. Enkarot/inkaroti
___________________________________
Sufuria. Emoti
Kikombe. Enkobo
Kipekecho. Orkipire
Sahani. Esaani
Chujio. Esilet
Beseni. Arkarai
Tochi. Ositimu
Kifuniko. Esiote
Nguo. Irkarash
Mlima. Oldonyo
Pori. Entim
Ardhi. Enkop
Majani. Inkujit
Miti. Irkeek
Kuni. Irkeek
Vumbi. Enterit
Udongo. Inkulukon
Tope. Esarng'ab
Bwawa. Elwane
Kisima. Oltilali
Njia. Enkitoi
Mto. Orkeju
Mawe. Isoitok
Boma. Enkang'
Gari. Engarrim
Baiskeli. Embasikeli
Pikipiki/bodaboda. Orpikipiki
Barabara. Orbarabara
Pote. Orgisoi
Mtu. Oltung'ani
Mtoto. Enkerai
Baba. Papaai
Mama. Yeiyo
Babu. Nkakui
Bibi. Koko
Mjomba. Alakuya
Jirani. Elatia
Shemeji. Paahe
Mama mkwe. Enkaputani
Baba mkwe. Alaputani
Mvulana. Alaiyeni
Msichana. Entito
Shoka. Entolu
Jembe. Orkembe
Panga. Osinkia
Wembe. Eembe
Mkuki. Embere
Viatu. Inamuka
Sime. Alalem
Kisu. Enkalem
Kiti. Olorika
Shamba. Enkurma
Kanisa. Kanisa
Biblia. Embibilia
Kalamu. Arkalamu
Penzeli. Orpenzeli
Dawati. Aldawati
Daftari. Endaftari
Rula. Erula
Shule. Shule
Rangi. Aranki
Jifunze. Inteng'enwoi
Hesabu. Enkikena
Nzi. Ilajang'ak
Nyuki. Ilotoro
Nge. Enkulupa
Kitanda. Errwat
Mswaki. Enkike
Shanga. Iltureh/imusitani
Buibui. Esurisuri
Mdudu. Orkurto
Kichwa. Elukunya
Nywele. Irpapiti
Uso. Enkomom
Macho. Inkonyek
Pua. Inkumeshi
Shavu. Eseder
Mdomo. Enkutuk
Ulimi. Orng'ejep
Meno. Ilala
Mate. Inkamulak
Mapengo. Enyiriri
Jino. Altagiligili
Masikio. Inkiyaa
Kisogo. Orkodonyo
Shingo. Orgos
Makamasi. Orkuluk
Mishipa. Ing'onyo
Mifupa. Iloik
Kifua. Orgoo
Mapafu. Ilaras
Mgongo. Ongoriong'
Mkono. Enkaina
Vidole. Irkimojik
Kucha iloisotok
Tumbo. Enkoshoke
Kitovu. Asararwa
Magoti. Inkung'
Miguu. Inkejek
Twende. Maape
Wapi. Ai
Rudi. Tushukunye
Sirudi. Mashukunye
Kwanini. Kainyoo
Wimbo. Osinkolio
Imba. Taranya
Naomba kaomonu
Leta. Iyau
Peleka. Yawa
Kimbia. Kwata
Tule. Mainasa
Myumba. Enkaji
Pesa. iropiani
Elfu moja. Enchata
Elfu mbili. Inkeek are
Elfu tatu. Inkeek uni
Elfu nne. Inkeek ong'wan
Elfu tano. Inkeek imiet
Elfu sita. Inkeek ile
Elfu saba. Inkeek naapishana
Elfu nane. Inkeek isiet
Elfu tisa. Inkeek naaudo
Elfu kumi. Inkeek tomon
Ukimwi. Biitia
Mafua. Oloirobi
Kukohoa. Enkirroget
Mkojo. Inkulak
Nzuri. Sidai
Mbaya. Torrono
Wahi. Taseku
Mawingu. Inkatambo
Mvua. Enjan
Radi. Enkukurrukurr
Baridi. Irobi
Upepo. Enkijape
Ziwa. Enaipasha
Chawa. Ilahe
Jumamosi, 26 Oktoba 2019
KWANINI KUPATA UPENDO WA KWELI NI VIGUMU SANA?
Swali: "Kwa nini kupata upendo wa kweli ni vigumu sana?"
Jibu: Sisi sote tuna hamu ya kupenda na kupendwa. Tunapata ngazi tofauti za upendo kutoka kwa wazazi, ndugu, marafiki, na wengine. Lakini wengi wetu pia tunataka kupata mtu huyo maalum ambaye tunaweza kushiriki kiwango cha upendo zaidi. Kupata upendo wa kweli kunaweza kuonekana kuwa vigumu sana, na mara nyingi ni vigumu kuelewa ni kwa nini. Swali kubwa la kuzingatia kwanza ni, "ufafanuzi wangu wa upendo wa kweli ni nini?" Kuelewa ni nini tunachomaanisha kuwa "upendo wa kweli" kunaweza kutusaidia kuona ni nini tunachotafuta na kwa nini inafanya kazi au haifanyi kazi.
Jamii nyingi hutumia neno upendo kwa uhuru sana. Upendo mara nyingi huhusishwa na hisia kali ambazo, kwa kweli, ni za kibinafsi na zisizo za kawaida. Katika sinema nyingi na maonyesho ya televisheni, tunaona wahusika ambao wanafuata homoni zao na wanafanya ngono kabla ya ndoa. Huku "upendo" ukiwa umekita mizizi katika hisia nzuri au hisia za kimwili, ambayo hugeuka kwa urahisi kama ilivyoanzishwa. Hakuna chochote kibaya kwa kutaka kupata hisia nzuri kwa mtu tunayempenda; hata hivyo, ikiwa hiyo ndiyo msingi wa uhusiano, uhusiano huo uu katika shida. Ikiwa aina ya "upendo" tunayoona imeonyeshwa katika utamaduni wa hii leo unaojaa ngono ni nini tunachotafuta, haishangazi inaonekana vigumu kupata; sio upendo wa kweli tunaofuata lakini uzoefu ambao, kwa asili, hauwezi kudumu kwa muda mrefu.
Biblia inatoa picha tofauti ya upendo. Upendo wa kweli ni wa Mungu-kwa kweli, Yeye ni upendo (1 Yohana 4: 8) — na ndiye aliyeweka haja ya kupenda na kupendwa ndani yetu. Kwa hiyo, kuelewa mpango wake kwa upendo ni muhimu. Upendo wa kweli, kulingana na Biblia, umetokana na dhabihu, kujitolea, na msukumo wa kumsaidia mpendwa (ona Yohana 15:13). Upendo wa Mungu kwetu ulimchukua msalabani. Tuna hakika kwamba Yesu hakuwa na hisia "za furaha" juu ya njia yake msalabani (Luka 22: 42-44). Biblia inaelezea uhusiano wetu na Yesu kama ile ya bwana na bibi arusi (Mathayo 9:15, Waefeso 5:32). Upendo wa kimapenzi umeumbwa ili kuongoza na kukua ndani na kujitolea katika ndoa (Mwanzo 2:24) na inapaswa kuwekwa msingi katika upendo wa dhabihu (Waefeso 5:22, 25-28).
Idadi yoyote ya vitu inaweza kufanya usipate upendo wa kweli, kulingana na mpango wa Mungu, ni vigumu. Hapa tutazingatia vikwazo vidogo vingi ambavyo tunakabiliwa navyo:
Kufikiri kuwa kuna mtu mmoja tu "wa kweli" kwetu. Huu ni uongo ambao unaweza kutufanya tuogope kwamba tunaishi kwa chini kuliko bora. Kusubiri mpenzi "anayekufaa" kamili ajidhihirishe inaweza kusubiri muda mrefu. Yeyote tunachagua kuoa anakuwa mtu "anayetufaa" kwa sababu tumefanya ahadi ya maisha kwa mtu huyo. Biblia imepunguza nyanja: upendo wetu wa kweli lazima uwe muumini anayeishi kwa ajili ya Bwana (2 Wakorintho 6: 14-15); zaidi ya hayo, Mungu atatoa hekima na ufahamu (Yakobo 1: 5). Watu wa hekima na kiungu ambao wanatujua vizuri pia wanaweza kutoa mwongozo wa kupata upendo wa kweli.
Kufikiri kwamba mtu atatutimiza au atatimiza. Mungu pekee ndiye anayeweza kutimiza kweli, kwa hivyo hatuna haja ya kupata upendo wa kimapenzi kuwa na hisia ya kutimiza! Hakuna hata mmoja wetu aliye mkamilifu, na kutarajia mwanadamu mwingine asiye mkamilifu kukidhi mahitaji yote ni jambo lisilo la kweli, lisilo la afya, na inaweza kusababisha tu kukata tamaa.
Siko tayari kubadili au kukua. Ni rahisi kufikiri aina ya mtu tutayependa awe pia upendo, lakini ni jitihada gani sisi wenyewe tunazotumia kwa kuwa mtu wa aina hiyo? Sisi sote tuna masuala yetu wenyewe ambayo tunapaswa kushughulikia kwa msaada wa Mungu ili kuwa aina ya watu Yeye anataka tuwe. Inaweza kuwashawishi kufikiri kwamba kupata upendo wa kweli utaweza kutatua maswala hayo. Lakini kuwa na uhusiano wa karibu na mtu hakuwezi kutatua matatizo yetu; kuna uwezekano wa kuzifichua zaidi. Hii inaweza kuwa sehemu nzuri ya uhusiano, kama vile chuma hunoa chuma kingine (Mithali 27:17), ikiwa tuko tayari kubadili na kukua. Ikiwa hatujui kubadili, uhusiano huo utaharibika.
Jumamosi, 28 Septemba 2019
UKWELI KUMHUSU MUNGU
(1).
JE, UMEWAHI kuona jinsi ambavyo watoto huuliza maswali? Wengi wao huanza kuuliza maswali mara tu wanapojua kuongea. Wanakutazama wakiwa wamekodoa macho kwa hamu na kuuliza maswali kama vile: Kwa nini anga ni bluu? Kwa nini nyota zinametameta? Ni nani aliyewafundisha ndege kuimba? Huenda ukajaribu sana kujibu, lakini mara nyingi si rahisi. Hata baada ya kuwapa jibu bora, huenda bado wakauliza: Kwa nini?
2 Si watoto peke yao wanaouliza maswali. Tunapoendelea kukua, sisi huuliza maswali. Tunauliza maswali ili tupate mwongozo, tujue hatari tunazohitaji kuepuka, au kwa sababu tu tunataka kujua. Hata hivyo, inaonekana kwamba watu wengi huacha kuuliza maswali, hasa yaliyo muhimu zaidi. Wao huacha kutafuta majibu.
3. Kwa nini watu wengi hawajitahidi kupata majibu ya maswali muhimu zaidi?
3 Fikiria swali lililo katika jalada la kitabu hiki, maswali yaliyo katika utangulizi wa kitabu hiki, au yale yaliyo mwanzoni mwa sura hii. Hayo ni baadhi ya maswali muhimu zaidi unayoweza kuuliza. Hata hivyo, watu wengi hawajitahidi kupata majibu ya maswali hayo. Kwa nini? Je, Biblia ina majibu? Watu fulani hufikiri kwamba Biblia haieleweki. Wengine huogopa kuuliza maswali ili wasiaibishwe au kudharauliwa. Hali wengine huamua kwamba maswali hayo yanaweza kujibiwa tu na viongozi na walimu wa dini. Wewe unaonaje?
4, 5. Ni maswali gani muhimu zaidi tunayoweza kuuliza maishani, na kwa nini tutafute majibu?
4 Bila shaka ungependa kupata majibu ya maswali muhimu zaidi maishani. Haikosi, nyakati nyingine wewe hujiuliza: ‘Maisha yana kusudi gani? Je, kusudi pekee la maisha ni kuzaliwa, kuzeeka, na kufa? Kwa kweli Mungu ana utu gani?’ Ni vizuri kuuliza maswali kama hayo, na ni muhimu kutafuta majibu yenye kuridhisha na yenye kutegemeka bila kukata tamaa. Yule mwalimu mashuhuri, Yesu Kristo, alisema hivi: “Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata; endeleeni kupiga hodi, nanyi mtafunguliwa.”—Mathayo 7:7.
5 ‘Ukiendelea kutafuta’ majibu ya maswali hayo muhimu, utafaidika sana. (Methali 2:1-5) Hata uwe umeambiwa nini na watu wengine, kuna majibu, na unaweza kuyapata katika Biblia. Majibu hayo si magumu, yasiyoeleweka. Isitoshe, yatakupa tumaini na shangwe. Na yanaweza kukusaidia kuishi maisha yenye kuridhisha sasa. Kwanza, na tufikirie swali moja ambalo limewahangaisha watu wengi.
JE, MUNGU ANA HURUMA NA JE, ANAJALI?
6. Kwa nini watu wengi wanafikiri kwamba Mungu hajali wanadamu wanapoteseka?
6 Watu wengi hujibu hapana. Wanasema, ‘Ikiwa Mungu anajali, ulimwengu ungekuwa tofauti sana.’ Leo, ulimwengu umejaa vita, chuki, na mateso. Isitoshe, kila mmoja wetu huwa mgonjwa, huteseka, na kufiwa na wapendwa wake. Ndiyo sababu watu wengi husema, ‘Ikiwa Mungu anatujali na kuhangaikia matatizo yetu, kwa nini hazuii mambo hayo yasitupate?’
7. (a) Walimu wa dini wamewafanyaje watu wengi wafikiri kwamba Mungu hana huruma? (b) Biblia inafundisha nini hasa kuhusu majaribu ambayo huenda yakatupata?
7 Isitoshe, nyakati nyingine walimu wa dini huwafanya watu wafikiri kwamba Mungu hana huruma. Jinsi gani? Msiba unapotokea, wanasema ni mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, walimu hao wanamlaumu Mungu kwa sababu ya mambo mabaya yanayotukia. Je, huo ndio ukweli kumhusu Mungu? Biblia inafundisha nini hasa? Andiko la Yakobo 1:13linajibu: “Mtu akiwa chini ya jaribu, yeye asiseme: ‘Mungu ananijaribu.’ Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na mambo maovu wala yeye mwenyewe hamjaribu yeyote.” Kwa hiyo, Mungu hasababishi kamwe uovu ambao unaona ulimwenguni. (Ayubu 34:10-12) Ni kweli kwamba anaacha mambo mabaya yatukie. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya kuacha jambo litukie na kulisababisha.
8, 9. (a) Unaweza kutumia mfano gani kuonyesha tofauti iliyopo kati ya kuacha uovu uwepo na kuusababisha? (b) Kwa nini si haki kumlaumu Mungu kwa kuwaacha wanadamu wafuate njia isiyofaa?
8 Kwa mfano, wazia baba mwenye hekima na busara aliye na mwana ambaye tayari ni mtu mzima na bado anaishi nyumbani kwa wazazi wake. Mwana huyo akiasi na kuamua kuondoka nyumbani, baba yake hamzuii. Mwana huyo anaishi maisha mapotovu na kupata matatizo. Je, baba ndiye aliyesababisha matatizo ya mwanaye? Hapana. (Luka 15:11-13) Vivyo hivyo, Mungu hawazuii wanadamu wakishaamua kufuata njia isiyofaa, hata hivyo hasababishi matatizo yanayowapata. Kwa hiyo, basi, si haki kumlaumu Mungu kwa sababu ya matatizo yote yanayowapata wanadamu.
9 Mungu ana sababu nzuri za kuwaacha wanadamu wafuate njia isiyofaa. Akiwa Muumba wetu mwenye hekima na nguvu, hahitaji kutueleza sababu hizo. Hata hivyo, Mungu hutueleza kwa sababu ya upendo. Utajifunza kuhusu sababu hizo katika Sura ya 11. Lakini uwe na hakika kwamba Mungu hasababishi matatizo yanayotupata. Badala yake, anatupa tumaini pekee la utatuzi!—Isaya 33:2.
10. Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu ataondoa madhara yote yanayotokana na uovu?
10 Isitoshe, Mungu ni mtakatifu. (Isaya 6:3) Hilo linamaanisha kwamba yeye ni safi wala hana uovu hata kidogo. Kwa hiyo, tunaweza kumtumaini kabisa. Hatuwezi kuwatumaini wanadamu ambao nyakati nyingine wanakuwa wafisadi. Hata wanadamu wenye mamlaka ambao ni wanyoofu zaidi mara nyingi hawana uwezo wa kuondoa madhara yanayosababishwa na watu wabaya. Lakini Mungu ana nguvu zote. Anaweza na ataondoa madhara yote yanayowapata wanadamu kwa sababu ya uovu. Mungu atakapochukua hatua, atakomesha uovu milele!—Zaburi 37:9-11.
MUNGU ANAHISIJE KUHUSU UKOSEFU WA HAKI?
11. (a) Mungu anahisije kuhusu ukosefu wa haki? (b) Mungu anahisije kuhusu kuteseka kwako?
11 Mungu anahisije kuhusu mambo yanayoendelea ulimwenguni na maishani mwako? Kwanza kabisa, Biblia inafundisha kwamba Mungu ni “mpenda-haki.” (Zaburi 37:28) Kwa hiyo anapendezwa sana na mambo yanayofaa na kuchukizwa na mambo yasiyofaa. Anachukia ukosefu wa haki wa kila namna. Biblia inasema kwamba Mungu ‘aliumia moyoni mwake’ uovu ulipokuwa mwingi duniani wakati uliopita. (Mwanzo 6:5, 6) Mungu hajabadilika. (Malaki 3:6) Bado anachukia kuona mateso yanayoendelea ulimwenguni pote. Pia, Mungu anachukia kuona watu wakiteseka. Biblia inasema, “yeye anawajali ninyi.”—1 Petro 5:7.
Biblia inafundisha kwamba Yehova ni Muumba wa ulimwengu mwenye upendo
12, 13. (a) Kwa nini tuna sifa nzuri kama vile upendo, nao upendo unatufanya tuwe na maoni gani kuhusu ulimwengu? (b) Kwa nini unaweza kuwa na hakika kwamba Mungu atachukua hatua kuhusiana na matatizo ya ulimwengu?
12 Tunawezaje kuwa na hakika kwamba Mungu anachukia kuona watu wakiteseka? Uthibitisho mwingine ndio huu. Biblia inafundisha kwamba Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake. (Mwanzo 1:26) Kwa hiyo, tuna sifa nzuri kwa sababu Mungu ana sifa nzuri. Kwa mfano, je, wewe husumbuka unapowaona watu wasio na hatia wakiteseka? Ikiwa unasumbuka kwa sababu ya ukosefu huo wa haki, uwe na hakika kwamba Mungu husumbuka hata zaidi.
13 Jambo moja la pekee kuhusu wanadamu ni kwamba tuna uwezo wa kuonyesha upendo. Mungu pia ana sifa hiyo. Biblia inafundisha kwamba “Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:8) Tuna upendo kwa sababu Mungu ana upendo. Je, upendo ungekuchochea kukomesha mateso na ukosefu wa haki unaoona ulimwenguni? Kama ungekuwa na uwezo wa kufanya hivyo, je, ungeyakomesha? Bila shaka ungeyakomesha! Uwe na hakika kwamba Mungu atakomesha mateso na ukosefu wa haki. Ahadi zinazotajwa katika utangulizi wa kitabu hiki si ndoto tu au matumaini yasiyo na msingi. Bila shaka ahadi za Mungu zitatimia! Hata hivyo, ili kuamini ahadi hizo, unahitaji kujua mengi zaidi kumhusu Mungu anayezitoa.
MUNGU ANATAKA UMJUE
Unapotaka mtu akujue, unamwambia jina lako, sivyo? Mungu anatujulisha jina lake katika Biblia
14. Mungu anaitwa nani, na kwa nini tunapaswa kulitumia jina lake?
14 Ukitaka mtu akujue, unaweza kufanya nini? Utamwambia jina lako, sivyo? Je, Mungu ana jina? Dini nyingi hujibu kwamba jina lake ni “Mungu” au “Bwana,” lakini hayo si majina yake binafsi. Hayo ni majina ya heshima kama vile “mfalme” na “rais.” Biblia inafundisha kwamba Mungu ana majina mengi ya heshima. Baadhi ya majina hayo ni “Mungu” na “Bwana.” Hata hivyo, Biblia inafundisha pia kwamba Mungu ana jina lake binafsi, yaani, Yehova. Andiko la Zaburi 83:18linasema hivi: “Wewe, ambaye jina lako ni Yehova, wewe peke yako ndiye Uliye Juu Zaidi, juu ya dunia yote.” Ikiwa Biblia yako haina jina hilo, unaweza kutazama nyongeza “Jina la Mungu—Maana na Matumizi” ili ujue ni kwa nini. Ukweli ni kwamba jina la Mungu linapatikana mara elfu kadhaa katika hati za zamani za Biblia. Kwa hiyo, Yehova anataka ulijue jina lake na kulitumia. Tunaweza kusema kwamba anatumia Biblia kujitambulisha kwako.
15. Jina Yehova linamaanisha nini?
15 Mungu alijipa jina lenye maana. Jina lake, Yehova, linamaanisha kwamba anaweza kutimiza ahadi yoyote anayotoa na kufanya jambo lolote analokusudia. * Jina la Mungu ni la pekee, halina kifani. Ni lake peke yake. Yehova ni wa pekee katika njia mbalimbali. Jinsi gani?
16, 17. Tunaweza kujifunza nini kumhusu Yehova kutokana na majina haya ya heshima: (a) “Mweza-Yote”? (b) “Mfalme wa umilele”? (c) “Muumba”?
16 Tuliona kwamba andiko la Zaburi 83:18 linasema hivi kumhusu Yehova: “Wewe peke yako ndiye Uliye Juu Zaidi.” Vivyo hivyo, Yehova peke yake ndiye anayeitwa “Mweza-Yote.” Andiko la Ufunuo 15:3 linasema: “Matendo yako ni makuu na ya ajabu, Yehova Mungu, Mweza-Yote. Njia zako ni za uadilifu na za kweli, Mfalme wa umilele.” Jina “Mweza-Yote” linatufundisha kwamba Yehova ndiye mwenye nguvu zaidi kuliko wote. Nguvu zake hazina kifani; ni nyingi sana. Nalo jina “Mfalme wa umilele” linatukumbusha kwamba Yehova ni wa pekee katika njia nyingine. Yeye peke yake ndiye amekuwapo nyakati zote. Andiko la Zaburi 90:2 linasema: “Tangu wakati usio na kipimo mpaka wakati usio na kipimo [au, milele] wewe ni Mungu.” Maneno hayo yanatuchochea tumheshimu, sivyo?
17 Pia, Yehova ni wa pekee kwa sababu yeye peke yake ndiye Muumba. Andiko la Ufunuo 4:11linasema: “Unastahili, Ee Yehova, naam, Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu, kwa sababu uliumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.” Kila kitu unachoweza kuwazia, iwe viumbe wa roho mbinguni ambao hawaonekani, nyota zinazotapakaa katika anga la usiku, matunda yanayokua mitini, au samaki walio baharini na kwenye mito, vyote vipo kwa sababu Yehova ndiye Muumba!
JE, UNAWEZA KUMKARIBIA YEHOVA?
18. Kwa nini watu fulani wanahisi kwamba hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, lakini Biblia inafundisha nini?
18 Kusoma kuhusu sifa za Yehova za ajabu, huwafanya watu fulani wamwogope. Wanahisi kwamba Mungu yuko juu sana wasiweze kumkaribia, nao ni duni machoni pake. Lakini je, hayo ni maoni yanayofaa? Biblia haifundishi hivyo. Inasema hivi kumhusu Yehova: “Hayuko mbali sana na kila mmoja wetu.” (Matendo 17:27) Hata Biblia inatuhimiza hivi: “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.”—Yakobo 4:8.
19. (a) Tunawezaje kuanza kumkaribia Mungu, nasi tutapata faida gani? (b) Ni sifa gani za Mungu zinazokuvutia zaidi?
19 Unawezaje kumkaribia Mungu? Kwanza kabisa, endelea kujifunza kumhusu kama unavyofanya sasa. Yesu alisema: “Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na juu ya yule uliyemtuma, Yesu Kristo.” (Yohana 17:3) Naam, Biblia inafundisha kwamba kujifunza kumhusu Yehova na Yesu huongoza kwenye “uzima wa milele”! Kama tulivyoona, “Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:16) Pia, Yehova ana sifa nyingine nyingi nzuri zenye kuvutia. Kwa mfano, Biblia inasema kwamba Yehova ni “Mungu mwenye rehema na neema, si mwepesi wa hasira naye ni mwingi wa fadhili zenye upendo na kweli.” (Kutoka 34:6) Yeye ni ‘mwema na yuko tayari kusamehe.’ (Zaburi 86:5) Mungu ana subira. (2 Petro 3:9) Yeye ni mshikamanifu. (Ufunuo 15:4) Kadiri unavyozidi kujifunza mengi katika Biblia, ndivyo utakavyozidi kujua jinsi Yehova ameonyesha sifa hizo na nyingine nyingi zenye kuvutia.
20-22. (a) Kwa kuwa hatuwezi kumwona Mungu, je, inamaanisha kwamba hatuwezi kumkaribia? Eleza. (b) Huenda watu fulani wasio na nia mbaya wakakusihi ufanye nini, lakini unapaswa kufanya nini?
20 Ni kweli kwamba huwezi kumwona Mungu kwa sababu yeye ni roho asiyeonekana. (Yohana 1:18; 4:24;1 Timotheo 1:17) Hata hivyo, ukijifunza kumhusu katika Biblia, utaujua utu wake. Kama mtunga-zaburi alivyosema, unaweza “kuuona uzuri wa Yehova.” (Zaburi 27:4;Waroma 1:20) Unapozidi kujifunza kumhusu Yehova, atakuwa halisi zaidi kwako nawe utampenda na kumkaribia zaidi.
Upendo wa baba kwa watoto wake unaonyesha upendo mkubwa zaidi ambao Baba yetu wa mbinguni anatuonyesha
21 Utaelewa hatua kwa hatua ni kwa nini Biblia inatufundisha kumwona Yehova kuwa Baba yetu. (Mathayo 6:9) Mbali na kwamba ametupa uhai, anataka tuwe na maisha bora iwezekanavyo, kama vile baba yeyote mwenye upendo angewatakia watoto wake. (Zaburi 36:9) Pia, Biblia inafundisha kwamba wanadamu wanaweza kuwa rafiki za Yehova. (Yakobo 2:23) Hebu wazia—wewe unaweza kuwa rafiki ya Muumba wa ulimwengu!
22 Unapoendelea kujifunza mengi zaidi katika Biblia, huenda watu fulani wasio na nia mbaya wakakusihi uache kujifunza. Huenda wakaogopa kwamba utabadili dini yako. Lakini usimruhusu mtu yeyote akuzuie kufanya urafiki pamoja na Mungu.
23, 24. (a) Kwa nini unapaswa kuendelea kuuliza maswali kuhusu mambo unayojifunza? (b) Ni habari gani itakayozungumziwa katika sura inayofuata?
23 Ni kweli kwamba kuna mambo ambayo hutaelewa mwanzoni. Unyenyekevu unahitajiwa ili kuomba msaada, lakini usisite kuuliza kwa sababu ya aibu. Yesu alisema kwamba ni vizuri kuwa mnyenyekevu kama mtoto mchanga. (Mathayo 18:2-4) Kama tujuavyo, watoto huuliza maswali mengi. Mungu anataka upate majibu. Biblia inawasifu watu waliokuwa na hamu ya kujifunza kumhusu Mungu. Waliyachunguza Maandiko kwa uangalifu ili kuhakikisha kwamba mambo waliyokuwa wakijifunza ni ya kweli.—Matendo 17:11.
24 Njia bora zaidi ya kujifunza kumhusu Yehova ni kuichunguza Biblia. Biblia ni tofauti na vitabu vingine vyote. Jinsi gani? Sura inayofuata itazungumzia habari hiyo.
Asante kwa kutembelea ukurasa huu Mungu akubariki sana
Jumatatu, 23 Septemba 2019
SIRI 5 KUBWA ZA MAFANIKIO
Kila binadamu ameumbwa na kiu ya kufanikiwa katika kila kitu anachofanya. Mafanikio ndio kilele cha mlima mkubwa wa maisha ambao umejengwa kwa misingi na ngazi za mihangaiko na mitihani ambayo unapaswa kuivuka ili upumzike kwenye kilele hicho.
Kwa bahati mbaya, unaposema ‘mafanikio’ wengi hufikiria kuhusu ‘utajiri’. Lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kati ya kuwa tajiri na kufanikiwa kiuchumi. Unaweza kuwa tajiri lakini ukawa bado hujafanikiwa. Kwa kuwa watu wanawaza utajiri kuwa ndio kigezo cha mafanikio hujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ajabu kwa lengo la kujizolea mali lakini mwisho huwa wanagundua kuwa hawajafanikiwa japo jamii inahisi wamefanikiwa.
Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind).
Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na ukosefu wa amani ya moyo. Hivyo, mafanikio ya njia ya mkato ni mafanikio feki yanayokuja na matatizo mengi mazito zaidi.
Kwa utangulizi huo mrefu, naamini utanielewa zaidi napokupitisha kwenye hizi ‘siri za wazi’ za mafanikio ya kweli katika maisha.
1. Jiamini
Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani. Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako. Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi.
2. Thubutu
Neno hili pia ni msingi wa pili mkuu wa mafanikio. Uoga wa kuthubutu ni kikwazo kikuu kinachowarudisha wengi nyuma na kujikuta hata kuanza safari ya mafanikio hawawezi. Jambo lolote zuri na kubwa huwa gumu kufanya na ni rahisi kuhisi haliwezekani. Usikubali kushindwa bila kujaribu. Thubutu kwa dhati na weka nguvu yako na akili yako yote katika uthubutu huo. Hata hivyo, katika uthubutu huu, unapaswa kupima vizuri ili uchukue ‘calculated risk’ na sio ‘just risk
3. Panga na tekeleza kwa vitendo
Kumbuka, ukishindwa kupanga ujue umepanga kushindwa. Kuwa na mipango inayopimika na kutekelezeka kwa kiwango cha juu. Usiwe na mipango tu mikubwa ambayo hata utekelezaji wake hauwezekani. Unapopanga fikiria wapi utapata rasilimali na jinsi ya kutelezeka, lakini pia mpango wako ukupe uwezo wa kuutathmini na kujipima mwisho wa kazi hiyo. Hata hivyo, mipango haitakuwa na maana kama hautaitekeleza kwa ufanisi. Ukishindwa kutekeleza mpango wako, rudi angalia ulipoteleza ili urekebishe na sio kuufuta mpango mzima bila sababu za msingi.
4. Tengeneza mtandao na wasiliana
Mtandao ni kama daraja au miundombinu ya kuyafikia mafanikio. Hakikisha haujifungii kwenye dunia yako peke yako. Hakikisha kila unaekutana naye na kupata nafasi ya kumfahamu kama mtu anayeweza kuwa sehemu ya daraja bora kwa namna moja au nyingine, anakuwa sehemu ya mtandao wako.
Lakini kuwa na mtandao wa watu pekee hautoshi kama hautawasiliana nao. Kuwasiliana na mtandao huo ni kuufanya uwe ‘active’ ili isionekane kama unawatafuta wakati ukiwa na shida tu. Aidha, unapaswa kujipima kwa kuangalia watu wangapi wanakufahamu wewe zaidi ya watu wangapi unaowafahamu. Kwa mfano: wewe unamfahamu Mkurugenzi wa kampuni ‘A’, Jiulize, je, yeye anakufahamu? Kama hakufahamu basi yeye sio sehemu ya mtandao wako.
Lakini pia, angalia mawasiliano yako ya siku, wangapi umeongea nao kuhusu wazo la biashara au kazi.
5. Kuwa mkweli na Mwaminifu
Hii ni siri kubwa zaidi ya zote, japokuwa nimeiweka mwishoni kati ya hizi tano. Usipokuwa mwaminifu na mkweli huku unaona mambo yako yanaenda vizuri unapaswa kushtuka mapema. Wewe ni kama mtu anaevuka ng’ambo ya pili huku akilivunja daraja. Mwisho wa siku utajikuta unaporomoka kabla hujafika unakotakiwa kufika.
Uaminifu utaimarisha mtandao wako kwa hali ya juu zaidi na utatafutwa kwa kuwa wewe utakuwa sehemu ya sababu ya mafanikio ya watu wengine. Kwa mfano, angalia namba ulizonazo kwenye simu yako ya mkononi. Je, ukitaka kumpigia simu dereva taxi majira usiku au hata muda wa kawaida utatumia vigezo gani? Bila shaka uaminifu na ukweli vitatangulia zaidi.
Kuwa mwaminifu na mkweli kwa kila mtu utakayefanya nae kazi, biashara au hata wakati mnafanya mambo ya kawaida ya kijamii kunakupa nafasi ya kuwa chaguo la kwanza kwa watu wanapohitaji huduma, bidhaa au rasilimali ambayo unayo.
Ukifuata kwa uhakika haya matano huku ukimkumbuka Mungu wako kwa kila jambo utafanikiwa kweli na kubaki na amani ya moyo.
JIFUNZE KUSAMEHE
Wewe na mwenzi wako mnapogombana, mnataja tena orodha ya makosa ya wakati uliopita, mnakumbushana mambo mabaya mliyotendeana zamani ambayo yalipaswa kusuluhishwa muda mrefu uliopita. Tatizo ni nini? Huenda mmoja wenu au nyote wawili hamjui jinsi ya kusamehe.
Mnaweza kujifunza kusameheana. Hata hivyo, kwanza, fikiria kwa nini huenda mume na mke wakaona ni vigumu kusameheana.
KWA NINI HILI HUTOKEA?
Mamlaka. Waume na wake fulani huamua kutosamehe ili wawe na kiasi fulani cha mamlaka juu ya wenzi wao. Halafu, wanapogombana, wanatumia matukio ya wakati uliopita kuwadhibiti wenzi wao.
Kinyongo. Mtu anapokosewa anaweza kuendelea kukumbuka jambo hilo kwa muda mrefu. Huenda mwenzi wa ndoa akasema ‘nimekusamehe’ lakini bado afungie kinyongo—na labda hata apange kulipiza kisasi.
Kukatishwa tamaa. Watu fulani huingia katika ndoa wakiamini kabisa kwamba maisha yao yatakuwa ya raha mustarehe. Kwa hiyo, kutoelewana kunapotokea, wanajiuliza inawezekanaje kwamba mwenzi waliyefikiri anawafaa kabisa ana maoni tofauti na yao. Matarajio yasiyo halisi yanaweza kumfanya mtu awe na kawaida ya kutafuta makosa na asiwe tayari kusamehe.
Kutoelewa kusudi la kusamehe. Watu wengi hukataa kuwasamehe wenzi wao kwa sababu hawaelewi kusudi la kusamehe. Kwa mfano, wao hujiambia:
Nikimsamehe, nitakuwa nikipunguza uzito wa kosa.
Nikimsamehe, lazima nisahau alichotenda.
Nikimsamehe, atanitendea vibaya hata zaidi.
Kwa kweli, kusamehe hakumaanishi mambo yatakuwa kama yalivyotajwa hapo juu. Hata hivyo, bado inaweza kuwa vigumu kusamehe—hasa kwa watu wenye uhusiano wa karibu kama mke na mume.
MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA
Fahamu maana ya kusamehe. Katika Biblia, nyakati nyingine neno “samehe” linamaanisha “kuachilia.” Kwa hiyo, kusamehe hakumaanishi kwamba mara zote unapaswa kusahau mambo yaliyotokea au kupunguza uzito wa kosa. Nyakati nyingine kunaweza kumaanisha kuachilia mambo kwa manufaa yako na ya ndoa yako.
Tambua matokeo ya kutosamehe. Wataalamu fulani wanasema kwamba kuweka kinyongo kunaweza kusababisha matatizo ya kimwili na kihisia, yanayotia ndani kushuka moyo na kupanda kwa shinikizo la damu—isitoshe kunaweza kuharibu ndoa yako. Biblia ina sababu nzuri inaposema hivi: “Iweni wenye fadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma nyororo, mkisameheana kwa hiari.”—Waefeso 4:32.
Tambua faida za kusamehe. Roho ya kusamehe inawasaidia watu waliofunga ndoa waamini kwamba mwenzi wao hakuwa na nia mbaya alipowakosea na hivyo kuepuka kuhesabu mabaya. Kufanya hivyo kutawasaidia kujenga mazingira yanayozuia chuki na kuruhusu upendo kukua.—Kanuni ya Biblia: Wakolosai 3:13.
Ona mambo kihalisi. Ni rahisi zaidi kusamehe ikiwa unamkubali mwenzi wako jinsi alivyo, licha ya upungufu wake. Kitabu Fighting for Your Marriage (Jinsi ya Kuiokoa Ndoa Yako) kinasema kwamba unapokazia fikira udhaifu wa mwenzi wako huenda ukasahau sifa zake nzuri. Kitabu hicho kinauliza hivi: “Ni nini hasa ambacho ungependa kukazia fikira kwa kuwa tayari umefunga ndoa?” Kumbuka, hakuna mtu mkamilifu—kutia ndani wewe.—Kanuni ya Biblia: Yakobo 3:2.
Uwe mwenye kukubali sababu. Wakati ujao unapokasirishwa na jambo fulani ambalo mwenzi wako amesema au kufanya, jiulize hivi: ‘Je, kweli jambo hilo ni muhimu? Je, lazima niombwe msamaha, au naweza kupuuza kilichotokea na kusonga mbele?’—Kanuni ya Biblia: 1 Petro 4:8.
Ikiwa ni lazima, zungumzieni jambo hilo. Eleza kwa utulivu jambo lililokukasirisha, na kwa nini unahisi hivyo. Usishuku kwamba mwenzi wako ana nia mbaya na usishikilie sana maoni yako, kwa kuwa kufanya hivyo kutamfanya tu mwenzi wako ajitetee. Badala yake, eleza tu jinsi matendo ya mwenzi wako yalivyokuathiri.
TATIZO SIO MTAJI NI WEWE TU
Hawa ni wale wenye shauku kubwa moyoni mwao kufanya jambo la pekee na hawafanyi lakini ukiwauliza watakupangia sababu nyingi za kuhalalisha ...
-
KIMAASAI to ENGLISH pronounced hello= supai hello all = enda supai pooki thank you very much=ashe oleng' ve...
-
UKIKUTA MKUKI NJE KWA WAMASAI KUNA MAANA GANI?? LEO NAFAFANUA. Kwa muda mrefu Sana nimesikia dhana potofu ikisemwa na watu wasio na uel...
-
Jinsi ya Kuishi Maisha Yenye Furaha “Nitakuwa na furaha nikifunga ndoa na kupata watoto.” “Nitakuwa na furaha nikimiliki nyumba yangu mw...





